
KATIKA muda wa kipindi cha miaka miwili iliyopita, nchi tisa kati ya nchi kumi zimerudi nyuma kwenye Fahirisi ya Maendeleo ya Binadamu ya Umoja wa Mataifa.
Mapolomoko ya vitu hivyo yameonyesha kusababishwa na Uviko-19, vita vya Ukraine na athari za mabadiliko ya hali ya hewa katika nchi hizo na kusababisha maendeleo ya ulimwengu Kwenda kinyume na mategemeo.
Fahirisi ya Maendeleo ya Binadamu ilizinduliwa mwaka 1990 katika jitihada za kuangalia zaidi ya Pato la Taifa kama kipimo cha ustawi.

Uswizi iko kileleni mwa faharasa mwaka huu ikiwa na umri wa kuishi miaka 84, wastani wa miaka 16.5 iliyotumika katika elimu na wastani wa mshahara wa dola 66,000.
Kwa upande mwingine wa kiwango hicho ni Sudan Kusini ambapo umri wa kuishi ni 55, watu hutumia miaka 5.5 tu shuleni kwa wastani na kupata dola 768 kwa mwaka.
Imeandikwa: leocardia Charles kwamsaada wa mitandao.