×

Waziri Mkuu Liz Truss Amtangaza King Charles III Kuwa Mtawala Mpya wa Nchi ya Uingereza

King Charles III.
Kufuatia kifo cha mtawala wa Uingereza Malkia Elizabeth II, Waziri Mkuu wa nchi hiyo amemtangaza Mrithi wa nafasi ya kiutawala ya Malkia ambapo katika taarifa yake Waziri Mkuu wanchi hiyo Liz Truss amemtangaza Prince Charles III (King Charles III) kuwa ndiye mtawala mpya wa nchi ya Uingereza.
Waziri Mkuu Uingereza, Liz Truss.

 

Prince Charles III atahudumu kama Mfalme wa Uingereza lakini pia atahudumu kama kiongozi mkuu wa Jumuiya ya Madola.

“Leo taji la kifalme linahama, kama lilivyofanya kwa zaidi ya miaka elfu moja iliyopita, na linakwenda kwa mfalme wetu mpya, mkuu wetu mpya wa nchi, Mfalme Charles wa tatu”

 

Aidha, mbali na Kutoa taarifa hiyo Waziri Mkuu Liz Truss alisema kwamba wanaungana pamoja na familia ya kifalme kuomboleza kifo cha mama wa mfalme wao mpya na wanapoomboleza, ni lazima wakusanyike pamoja kama ili kumuunga mkono, ili kumsaidia kubeba madaraka hayo makubwa ambayo kwa sasa anayabeba kwa ajili yao wote.

Leave a Comment