×

Beki wa Man City Benjamin Mendy Akutwa Hana Hatia Kesi ya Ubakaji

                                     Beki wa Manchester City Mfaransa Benjamin Mendy

STAA wa Manchester City Benjamin Mendy amekutwa hana hatia kwenye kesi ya ubakaji  wa binti wa miaka 19, Mfaransa huyo  alituhumiwa kutenda kosa hilo katika jumba lake la kifahari huko Cheshire mnamo Julai 24 mwaka jana.

Mahakama ilimuondolea shtaka hilo kwa amri ya hakimu katika Mahakama ya Chester baada ya upande wa mashtaka kutotoa ushahidi zaidi.

Jumanne Jaji Stephen Everett aliamuru mahakama kuwaondolea washtakiwa makosa hayo baada ya upande wa mashtaka kutotoa ushahidi zaidi na mashtaka rasmi ya kutokuwa na hatia kuingizwa.

Louis Saha

Rafiki yake Louis Saha Matturie, 41, pia alikutwa hana hatia kwa maelekezo ya hakimu wa makosa mawili ya ubakaji na moja la unyanyasaji wa kingono dhidi ya mwanamke huyo.

Imeandikwa: Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa mitandao

Leave a Comment