×

TGNP na WiLDAF Watoa Mafunzo kwa ADA TADEA Namna ya Kuandaa Sera Zenye Mrengo wa Kijinsia

Mtafiti wa Masuala ya Siasa, Muwezeshaji na Mwelekezi, Hanif Tuwa (kulia) akitoa mafunzo hayo kwa viongozi wa Ada Tadea.

 

 

MTANDAO wa jinsia nchini, TGNP kwa kushirikiana na shirika la WiLDAF wametoa mafunzo kwa chama cha siasa cha Ada Tadea na kuwafundisha ya jinsi ya kutunga sera zenye mrengo wa kijinsia.

Washiriki wakiwa makini kupata mafunzo hayo.

 

Akizungumza na mwandishi wetu, Mtafiti wa masuala ya siasa, muwezeshaji na mwelekezi, Hanif Tuwa amesema lengo la mafunzo hayo kwa chama hicho ni sehemu ya muendelezo na harakati za TGNP kwa kushirikiana na Shirika la WiLDAF kuvijengea uwezo vyama vya siasa haswa katika mrengo wa kijinsia.

Mtafiti wa Masuala ya Siasa, Muwezeshaji na Mwelekezi, Hanif Tuwa akikazia jambo wakati akitoa mafunzo hayo.

 

Hanif ameendelea kusema kuwa kingine kilichowakutanisha kwenye mkutano huo ni kujadili na kuwajengea uwezo wa namna ya kuandaa sera za kijinsia ambazo zitatoa muongozo na hatua zote zitachukuliwa katika masuala ya program ndani ya chama.

Hanif aliendelea kusema;

 

“Kwa hiyo hii ni program inayochukua siku 7 ambapo tuna mijadala ya kupeana mbinu mbalimbali za kiuwezeshi kama vikundi kazi lakini mwisho wa siku tunategemea mchakato huu utaishia kwenye kuwepo kwa rasimu.

Mwenyeki wa wanawake wa Ada Tadea Dianarose Mhoja akizungumza baada ya kupata mafunzo hayo.

 

“Washiriki wetu katika mafunzo haya kimsingi wanatokea sekretarieti na vyombo vya juu vya maamuzi ya chama kwa idhini ya mwenyekiti na vikao rasmi vilivyopitisha mchakato huu.

 

“Nashukuru katika mafunzo haya muitikio umekuwa mzuri ambapo tumepata uwakilishi mzuri pia, tuna kinamama watatu na kinababa watatu.

Katibu Mkuu wa Ada Tadea, Salehe Msumari akizungumza baada ya kupata mafunzo hayo.

 

“Hii inatoa picha kuwa kile tunachokikusudia kina uwezekano mkubwa wa kutimia pengine katika namna ambayo hata sisi wenyewe hatukutarajia.” Alimaliza kusema Hanif.

 

Naye Mwenyekiti wa wanawake wa Ada Tadea, Dianarose Mhoja amesema anaishukuru TGNP kwa kuwapa mafunzo hayo ambayo anaamini yatawawezesha kutunga sera ipasavyo kwakuwa sera ndiyo roho ya chama.

Picha ya pamoja baada ya mafunzo.

 

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Chama cha Ada Tadea, Salehe Msumari amesema yeye anaishukuru sana TGNP kwa kuwapa mafunzo hayo ambayo anaamini yatawaamsha kinamama, walemavu na watu wengine kutoka makundi maalum katika masuala ya siasa na kuweza kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi mkuu ujao wa serikali za mitaa na hata uchaguzi mkuu.

Leave a Comment