
MABADILIKO ya hali ya hewa yanayosababishwa na binadamu huenda yakachangia mafuriko makubwa nchini Pakistan hivi karibuni, wataalam wanasema katika uchambuzi mpya wa kisayansi ambao uliangalia ni kiasi gani cha ongezeko la joto duniani kinapaswa kulaumiwa.
The World Weather Attribution, mkusanyiko wa wanasayansi wengi wa kujitolea kutoka kote ulimwenguni ambao hufanya uchunguzi wa wakati halisi wa hali mbaya ya hewa, walitoa ripoti yao Alhamisi.
Utafiti huo ulisema ongezeko la joto duniani sio sababu kubwa ya maafa makubwa ya mafuriko ambayo wakati fulani yalizamisha theluthi moja ya nchi na kuathiri watu milioni 33, kuua zaidi ya elfumoja miatano hadi sasa na kuharibu zaidi ya nyumba milioni moja.

Utafiti huo ulisema kuwa “Tukio kama hilo pengine lingekuwa na uwezekano mdogo sana katika ulimwengu bila uzalishaji wa gesi chafu unaosababishwa na binadamu, ikimaanisha kuwa mabadiliko ya hali ya hewa yana uwezekano wa kufanya mvua kubwa kunyesha”.
Imeandikwa: leocardia Charles kwa msaada wa mitandao.