×

Waliovamia Uwanja wa Simba Wapewa Siku 60 na RC Makalla Kuondoka

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla

MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla, amewataka wakazi tisa waliovamia uwanja wa klabu ya simba uliopo eneo la Bunju jijini Dar es salaam kuhama mara moja huku akiwapa siku 60 kuondoka katika eneo hilo.

 

Makalla amewataka wakazi hao kuondoka katika eneo hilo kwa kuwa Klabu ya Simba ilipewa kihalali na Rais Msataafu Jakaya Kikwete kujenga Uwanja wake kama Klabu unaojulikana kwa jina maarufu kama Mo Simba uliopo katika eneo hilo la Bunju.

 

Pia ameiruhusu Klabu hiyo kuendelea na ujenzi wa ukuta kuzunguka uwanja huo uliokuwa umesimama kwa muda kutokana na uvamizi huo.

Uwanja wa Simba uliopo Bunju, Dar es Salaam (Mo Arena)

Mkuu wa Mkoa huyo aliyasema hayo wakati alipotembelea eneo hilo kukagua uvamizi wa wakazi hao, huku akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe pamoja na viongozi wengine wa Klabu ya Simba.

 

 

Kwa upande wake DC Gondwe, alisema kuwa anatii agizo la Makalla la kuwapa Simba haki yao kwa sababu uamuzi huo ulifanywa na Rais Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete.

Imeandikwa na: Oswald Mwesiga kwa msaada wa mitandao.

Leave a Comment