
MSHAMBULIAJI wa Klabu ya Manchester City Erling Haalnd ameendeleza moto wake wa kufania nyavu katika michezo ya Ligi Kuu ya Uingereza ambapo leo katika mchezo dhidi ya Wolves amefanikiwa kufunga bao lake la 11 kwenye Ligi Kuu ya Uingereza.
Haalnd ambaye amechukua tuzo ya mchezaji bora wa mwezi uliopita amekuwa kwenye kiwango cha hali ya juu tangu alipokamilisha uhamisho wake wenye thamani ya paundi milioni 51 akitokea nchini Ujerumani katiuka klabu ya Borussia Dortmund.

Manchester City imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Wolves, mabao ambayo yamefungwa na Jack Grealish, Erling Halaand pamoja na Phil Foden.

Kwa matokeo hayo Manchester City inakwea hadi nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza ikiwa na jumla ya alama 17 huku ikiwa tayari imecheza michezo 7, nafasi ya pili inashikiliwa na klabu ya Arsenal yenye jumla ya alama 15 na ikiwa tayari imecheza michezo 6.