×

Rais Biden, Samia Wawasili London, Viongozi 500 Kutoa Heshima za Mwisho kwa Malkia

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan alivyowasili katika uwanja wa Ndege wa Luton tarehe 17 Septemba, 2022 kwa ajili ya kuhudhuria mazishi ya Malkia Elizabeth II wa Uingereza yatakayofanyika tarehe 19 Septemba, 2022 Jijini London.

 

Rais wa Marekani Joe Biden na Samia Suluhu wa Tanzania ni miongoni mwa viongozi waliowasili jijini London tayari kuhudhuria mazishi ya Malkia Elizabeth II siku ya Jumatatu.

 

Viongozi hao ni miongoni mwa wakuu 500 na viongozi wa kigeni wengi wanaokuja London kwa tukio linaliwakutanisha viongozi wa ulimwengu wengi zaidi kuonekana kwa pamoja kwa miongo kadhaa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Muwakilishi wa Mfalme Charles III, Cynthia Gresham wa Uingereza pamoja na Balozi wa Tanzania nchini humo Dkt. Asha-Rose Migiro mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Luton tarehe 17 Septemba, 2022 kwa ajili ya kuhudhuria mazishi ya Malkia Elizabeth II wa Uingereza yatakayofanyika tarehe 19 Septemba, 2022 Jijini London.

Mawaziri wakuu wa Canada, Australia na New Zealand tayari wako Uingereza.

Mzozo unazingira baadhi ya wageni waalikwa, kama vile Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed Bin Salman.

Mbali na Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese na Waziri Mkuu wa New Zealand Jacinta Ardern, viongozi wengine wa Jumuiya ya Madola wanaotarajiwa kuhudhuria ni pamoja na Waziri Mkuu wa Bangladesh Sheikh Hasina na Rais wa Sri Lanka Ranil Wickremesinghe.

 

India itawakilishwa na Rais Droupadi Murmu.

Viongozi walioalikwa leo watapata nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho huko Westminster na kutia saini kitabu cha maombolezo.

MAzishi ya kitaifa ya Malkia Elizabethi II yatafanyika kesho Jumapili kwenye kanisa la Westminstyer Abbey, London, kabla ya mwili wake kulazwa kwenye kasri la Windsor.

Leave a Comment