
MFUKO wa Kimataifa wa Kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria umepata dola bilioni14.25kama ufadhili mpya muhimu, baada ya miongo kadhaa ya maendeleo dhidi ya magonjwa kuharibiwa na janga la COVID-19.
Rais wa Marekani Joe Biden, ambaye alikuwa mwenyeji wa mkutano huo mjini New York kando ya mkutano wa ngazi ya juu wa kila mwaka wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA), alisema ufadhili huo kiasi kikubwa zaidi kuwahi kuahidiwa kwa shirika la afya la kimataifa ni muhimu katika kupambana na magonjwa.

Biden alisema “Huu ni uwekezaji ambao utaokoa maisha mengine milioni ishirini, kupunguza vifo vya magonjwa haya kwa asilimia 64 katika miaka minne ijayo”.
Mfuko huo ni muungano wa umma/binafsi ulioanzishwa mwaka 2002, unatafuta dola bilioni18 kwa mzunguko wake wa ufadhili wa miaka mitatu kutoka kwa serikali, mashirika ya kiraia na sekta ya kibinafsi. Kabla ya mkutano wa Jumatano tayari ilikuwa imeongeza zaidi ya theluthi moja ya jumla.
Imeandikwa: leocardia kwamsaada wa mitandao.