×

Rayvanny Ajutia Kumpenda Paula Kajala Achukua Uamuzi Mgumu, Rafiki Yake Afunguka

 

Staa wa muziki nchini Tanzania na bosi wa Lebo ya Next Level Music, Rayvanny au Vanny Boy akiwa na Paul.

Rayvanny au Vanny Boy; ni staa wa muziki nchini Tanzania na bosi wa Lebo ya Next Level Music ambaye anadaiwa kujuta kumpenda Paula Kajala, IJUMAA limedokezwa.

 

Kwa mujibu wa marafiki wa Rayvanny, suala la jamaa huyo kumpenda Paula lilikuwa linamnyima amani ya nafsi na akili na aliamua kuchukua uamuzi mgumu kisha kuanza safari ya matumaini ya kuvunja penzi lake na binti huyo wa kambo wa msanii Harmonize.

 

Rayvanny au Chui pia anawashauri watu kutofanya mfananisho wa mapenzi na chakula kwani ni vitu viwili tofuati.

Rayvanny ambye ni baba wa mtoto mmoja, miaka michache nyuma alimbwaga aliyekuwa baby mama wake, Faima, lakini sasa amerejesha majeshi wanamlea mtoto wao pamoja.

 

Kabla ya kuthibitisha kuachana na Paula, Rayvanny alisema hakuna mtu anayepaswa kuwachanganya kutokana na kuona ukweli wa mambo.

 

Watu hao wanasema kuwa, Rayvanny amekuwa akisisitiza kuwa, baada ya miezi michache ya kupata mapenzi hatimaye akapata amani ya moyo wake na kuachana na uhusiano wake na Paula.

 

“Usiruhusu mapenzi yakuchanganye, usifananishe mapenzi na chakula, nilifanya amani na moyo wangu na kukatisha uhusiano wangu na Paula,” anasema Rayvanny.

 

Ingawa hakuingia katika maelezo kuhusu kutengana kwa muda wote -kumwambia majuto yake inamaanisha tu kwamba alidhulumiwa na msichana huyo mbichi au hakuwahi kumpenda kama vile alivyotarajia.

 

Baadhi ya wale waliofuatilia penzi la Paula na Rayvanny wanaamini kwamba kutengana kwao au kufifia kwa penzi lao huwenda kulitokana na mama’ke Paula, Kajala Masanja kurudiana na msanii Harmonize ambaye awali walitengana kwa sababu ya huyo Paula kuviziwa na Harmonize.

 

Hivi karibuni Paula alidhibitisha kumkubali Harmonize kama baba yake wa kambo na hata kumsifia hadharani kwamba anajua kucheza muziki vizuri alipokuwa akicheza na mama’ke.

 

Harmonize pia ameonekana kumsifia sana Paula kwa kumuita binti yake na hata kutangaza biashara yake ya nguo.

Wiki iliyopita, Rayvanny alidokeza kwa video kwamba amerudiana na Faima baada ya kutengana kwa zaidi ya miaka mitatu ambapo wamekuwa wakishirikiana kulea mtoto wao.

Stori; Khadija Bakari, Dar

MAHABA NDANI YA LORI la MIZIGO, RAYVANNY na MREMBO WAKE WAWASHANGAZA TABORA..

Leave a Comment