×

Bilionea Musk Amshukia Zelensky Amtaka Atafute Suluhu ya Vita Dhidi ya Urusi

Volodymyr Zelensky

BILIONEA namba moja Duniani Elon Musk amemkingia kifua Rais wa Urusi Vladimir Putin na kumshutumu vikali Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kwa kushindwa kutetea maslahi mapana ya raia wake wanaoendelea kuteseka kutokana na mapigano nchini humo.

 

Elon Musk ametoa maneno hayo kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter akibainisha kuwa Zelensky anatakiwa kuchukua maamuzi sahihi ya kutafuta suluhu ya mgogoro huo kufuatia mikoa minne ya Donetsk, Kherson, Zaporizhzhia pamoja na Luhansk kuchukuliwa na Urusi kufuatia kura za maoni zilizopigwa na wananchi hao.

 

Mapema wakati vita inaanza Elon Musk alionesha nia ya kuiunga mkono Ukraine ambapo alitoa misaada mbalimbali ikiwemo huduma ya intaneti kuhakikisha kuwa nchi hiyo inaendelea kupata huduma hiyo muda wote wa mapigano.

Ukurasa wa Twitter wa Elon Musk

Kumekuwa na mapokeo mbalimbali juu ya kauli ya Musk huku Rais wa Ukraine Zelensky akimpiga kijembe Musk kwa kuweka ujumbe uliowataka watu kupiga kura kuonesha wanamkubali nani Elon Musk anayeiunga mkono Ukraine au yule anayeiunga mkono Urusi?

 

Kwa upande wa Kremlin taarifa zimepokelewa kwa mlengo chanya huku Msemaji wa Ikulu hiyo Dmitry Peskov akimpongeza Elon Musk na kubainisha kuwa kwa muda wote Urusi imekuwa tayari kwa ajili ya mazungumzo ya amani.

 

 

Leave a Comment