
NCHI ya Sudan imekuwa ikipitia majanga mbali mbali kama vile mafuriko, uvamizi wa kivita na njaa kiujumla na hii kupelekea wanafunzi kushindwa kuhudhuria shuleni au kuwepo na walimu wachache wa kufundisha.
Mafuriko na uvamizi wa kivita umepelekea uharibifu wa karibuni shule mia sita katika mwezi wa Agosti na Septemba na pia nchi ya Sudan kwa kuwa inakumbwa na umasikini basi magonjwa kama COVID-19 na kukosekana kwa chanjo imekuwa sababu moja wapo ya janga la wanafunzi kukosa shule.
Taarifa zinadai zaidi ya watoto milioni 2.4 hawaendi Shuleni kutokana na changamoto hizo.

Majimbo yaliyoathirika zaidi ni Darfur na Kassala ambapo kwa asilimia kubwa wanafunzi wamekosa kwenda shule na hata ambao wapo shule wanafanya vibaya katika masomo yao.” amenukuliwa akisema hivyo Ahmed el-safi ambaye ni Mwalimu nchini humo.
” Hawawezi kabisa kwenda shule wakati wakiwa na njaa wengi wao huishia kwenda masokoni na kuuza mifuko ya plastiki au kitu chochote ilimradi wapate mlo wa chakula wa siku”

Madarasa karibuni yote pamoja na nyumba za makazi ya watu wa Sudan zimebomoka kutokana na mafuriko ambayo yamepelekea kulala njaa na kulazimika kuingia sokoni na kufanya biashara za kuuza vitunguu na mifuko ya plastiki ilimradi wapate kitu cha kujikimu kimaisha, janga hili limekuwa sababu ya walimu na wanafunzi kwa kuingia sokoni na kufanya biashara na kuachana na shughuli zozote za mashuleni.
Imeandikwa na Arafat Ramadhan Salem kwa msaada wa mitandao