×

WHO: Afrika ina Kiwango Cha Juu Watu Wanaojitoa Uhai duniani

Shirika la Afya Duniani linasema Afrika ina kiwango kikubwa zaidi cha watu wanaojiua, Shirika hilo sasa limezindua kampeni ya mitandao ya kijamii ya kuzuia watu kujitoa uhai ikiwa na lengo la kuongeza ufahamu juu ya suala hilo.

 

Katika taarifa WHO limesema nchi sita za Afrika ni miongoni mwa nchi kumi zilizo na idadi kubwa ya watu wanaojitoa uhai kote duniani.

 

Shirika hilo lilibainisha kuwa matatizo ya afya ya akili yanachangia hadi 11% ya mambo ya hatari yanayohusiana na kujiua.

 

Mkurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika, Dk. Matshidiso Moeti alisema kujiua ni tatizo kubwa la afya ya umma lakini ni nadra kupewa kipaumbele katika mipango ya kitaifa ya afya.

 

Kampeni ya mitandao ya kijamii ilizinduliwa kabla ya Siku ya Afya ya Akili Duniani mnamo Oktoba 10, WHO inalenga kufikia watu milioni 10 kote barani humo.

 

Kwa mujibu wa  ripoti hiyo  inaonyesha kuwa daktari mmoja wa magonjwa ya akili  anahudumia wagonjwa mpaka laki tano (500,000) amesema  kwa kila wakazi 500,000 Hii ni mara 100 chini ya pendekezo la WHO.

Leave a Comment