×

SBL Kugawa Mbolea Bure kwa Wakulima Mkoani Songwe

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Waziri Kindamba akikagua banda la Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) wakati akizindua Maonyesho ya Siku ya Mbolea Duniani ambayo kitaifa yanafanyika Viwanja vya Komondo, Mlowo, Wilayani Mbozi mkoani Songwe. Wapili kushoto ni Kaimu Meneja wa TFC Kanjel Mloba wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Utengenezaji Mbolea ya SBL kutoka Kenya, Joe Kariuk.

 

 

KAMPUNI ya utengenezaji na usambazaji wa mbolea kutoka nchini Kenya SBL imetangaza neema kwa wakulima hapa nchini ambapo itatoa mfuko mmoja bure kwa wakulima watakaofika katika banda lake kwenye Maonyesho ya Siku ya Mbolea Duniani yanayofanyika kitaifa katika Viwanja vya Kimondo, Mlowo, Wilayani Mbozi, mkoani Songwe.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Utengenezaji Mbolea ya SBL kutoka Kenya, Joe Kariuk (kulia) akisalimiana na Kaimu Meneja wa TFC Kanjel Mloba kwenye Viwanja vya Komondo, Mlowo, Wilayani Mbozi.

 

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa maonyesho hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Joe Kariuk, amesema watakaonufaika na ofa hiyo ni wakulima watakaofika katika Banda la Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) na kununua kuanzia mifuko mitatu ya mbolea ya  SBL ndipo watapewa ofa hiyo ya mfuko mmoja bure.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Utengenezaji Mbolea ya SBL kutoka Kenya, Joe Kariuk akizungumza na wanahabari kuhusu ugawaji bure wa mbolea ya SBL kwenye maonyesho hayo.

 

Joe amesema SBL  dhamira ya kufanya hivyo jitihada za kuiunga mkono serikali ya Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kumuinua mkulima wa kitanzania;

 

“SBL imeonyesha ufanisi mkubwa nchini Kenya sasa tunataka hata hapa Tanzania wakulima wanufaike nayo ambapo kwa kuanzia tunatoa mfuko mmoja wa kilo 25 bure kwa wateja watakaofika katika maonyesho haya hapa Songwe,”alisemaJoe.

 

Amesema SBL kupitia TFC imeingiza mifuko 2500 ya mbolea hiyo ya organic ambayo ni rafiki wa mazingira;

 

“Mifuko hiyo 2500 imeingia Songwe na tutauza na kuigawa bure wananchi waje katika uwanja wa Kimondo Mlowo na wafike katika banda la TFC” ameongeza Joe.

 

Awali Kaimu Meneja wa Kampuni ya mbolea Tanzania TFC, Kanjel Mloba alisema mbolea hiyo ya SBL imeingizwa nchini kutokana na ubora wake na ufanisi wake ulioonekana huko Kenya.

 

“Pamoja na mbolea nyingine leo katika maonyesho haya TFC tumetambulisha mbolea hii ya SBL ambayo ni organic na ni mbolea nzuri hivyo tunahimiza wakulima kuitumia” amesema Kanjel.

 

Amesema TFC itaendelea kuhakikisha inawasaidia wakulima kuwafikishia mbolea bora ili kilimo chao kiwe chenye tija. Maonyesho hayo ya siku tatu yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania TFRS yameanza leo na yanatarajiwa kufungwa na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, Oktoba 13 mwaka huu.

Leave a Comment