×

Ukraine Kunasa Makombora Yakiwa Angani, Putin Kukutana na Rais wa Uturuki Erdogan

Ujerumani imeahidi kutoa msaada wa mitambo ya kisasa kwa Ukraine, ya kunasa makombora yakiwa angani.

Waziri wa ulinzni wa Ujerumani Christine Lambrecht amesema kwamba mitambo hiyo aina ya IRIS-T SLM, itawasili Ukraine katika siku chache zijazo.

 

“Misururu ya makombora iliyovurumishwa na Russia dhidi ya Ukraine inaonyesha umuhimu wa kutoa msaada wa ulinzi wa anga kwa Ukraine haraka iwezekanavyo,” amesema Lambrecht.

 

Makombora ya masafa marefu yaliyorushwa na Russia Jumatatu asubuhi, yameua rai ana kuharibu mfumo wa umeme katika sehemu kadhaa za Ukraine. Shambulizi hilo limejiri baada ya rais wa Russia Vladmir Putin kutangaza shambulizi lililotokea kwenye daraja linalounganisha Russia na Crimea, kuwa la kigaidi.

 

Rais wa Marekani Joe Biden ameshutumu Russia kwa kushambulia Ukraine kwa makombora ya masafa marefu, na kusema kwamba makombora hayo yalilenga raia.

Rais wa Uturuki Erdogan na Putin wa Russia walipokutana Sochi

Biden ametangaza kwamba Marekani na washirika wake wataendelea kuiwekea Russia vikwazo kutokana na vita vyake nchini Ukraine.

“Marekani inashutumu kwa nguvu zote mashambulizi ya makombora dhidi ya Ukraine hii leo katika sehemu mbalimbali za Ukraine ikiwemi mjini Kyiv. Mashambulizi hayo yameua rai ana kuharibu mifumo ya nchi bila faida yoyote ya kijeshi,” amesema Biden.

 

Marekani imetoa msaada wa zaidi yad ola bilioni 16.8 kwa Ukraine tangu uvamizi wa Russia ulipoanza Februari 24.

Marekani na washirika wake vile vile wamewekwa Russia vikwazo kadhaa za uchumi.

 

“Mashambulizi haya yanaoneza nguvu za kuendelea kuisaidia Ukraine hadi vita vitakapomalizika,” amesema Biden.

 

Rais wa Russia Vladmir Putin, amepanga kukutana na mwezake wa Uturuki Recep Tayip Erdogan wiki hii, kujailiana kuhusu pendekezo la Uturuki la kufanyika mazungumzo kati ya Russia na mataifa ya magharibi, kuhusu Ukraine.

 

Msemaji wa Russia Dmitry Peskov, ameambia waandishi wa habari kwamba Russia haijapata ishara yoyote ya kufanyika mazungumzo na mataifa ya magharibi, lakini hajakanusha ripoti kwamba Putin atajadiliana hoja hiyo na Erdogan, watakapokutana.

 

Putin na Erdogana wanatarajiwa kukutana wiki hii nchini Kazakhstan.

Uturuki ina uhusiano mzuri na Russia Pamoja na Ukraine na imeonekana kuwa mpatanishi anayefaa katika kumaliza vita vya Ukraine.

Uturuki ilisaidia kupatikana makubaliano ya kusafirisha nafaka kutoka Ukraine mwezi July.

Leave a Comment