×

Al Hilal Yawatumia Salamu Yanga, Yampiga Mtu Kama Ngoma 

Al Hilal imeshinda mabao 4-0 dhidi ya Wad Nobawi

 

KLABU ya Al Hilal wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani wameibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Wad Nobawi katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Sudan.

 

Mchezo unaofata Al Hilal SC watakuwa tena nyumbani kuvaana na Yanga SC katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika utakaopigwa siku ya Jumapili, Oktoba 16, 2022.

Kikosi cha Yanga

Utakumbuka katika mechi ya kwanza iliyochezwa Oktoba 8 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, timu hizo zilitoka sare ya kufungana 1-1

Leave a Comment