
Kocha wa zamani wa Yanga, Cedric Kaze ametangaza kuachana na klabu ya Namungo kama kocha Mkuu ikiwa ni siku moja tu baada ya Wauaji hao wa Kusini kupokea kichapo cha 3-2 dhidi ya Singida Big Stars.
“Nimeamua kuanzia leo kujiuzulu kama Kocha Mkuu wa Namungo; Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru sana Uongozi, wafanyakazi wenzangu wa Ufundi na wachezaji kwa ushirikiano wao na kujitolea.

“Nimalizie kwa kuwashukuru Mashabiki ambao wamekuwa wakiniunga mkono kila wakati na kuitakia Timu kila la heri kwa siku zijazo.” ameandika Kaze Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii.
Tangu ajiunge na ‘The Southern Killers’ Kaze ameiongoza klabu hiyo katika mechi sita za Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara na kuambulia sare tatu na vipigo vitatu. Namungo haijashinda mechi hata moja mpaka sasa msimu huu.