×

Odinga Amlaumu Ruto kwa Kupanda kwa Gharama ya Maisha Kenya

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga akihutubia waandishi wa habari baada ya kuasilisha kesi mahakamani kupinga matokeo ya kura za urais Agost 22 2022

 

Mgombea wa urais mara 5 bila mafanikio nchini Kenya Raila Odinga, ameendelea kuishutumu mahakama na tume ya uchaguzi, akidai kwamba alipokonywa ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti.

 

Akihutubia vijana wanaokusanyika kila mara jijini Nairobi, wanaojiita ‘bunge la wananchi’, Raila amesema kwamba “amenyamaza” tangu mahakama ilipomtangaza Dkt William Ruto kuwa mshindi wa uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti “lakini hajakubaliana na yaliyotokea”.

Rais wa Kenya William Ruto

‘Mliona ile sarakasi ya mwizi mwingine ambaye vile vile ni mwendawazimu anaitwa Chebukati. Ile tume yake wanne wamesema hapana hii sio kweli, wawili vile vile wamejificha na kubaki pekee yake. Baadaye anasemekana yeye ndiye shujaa. Halafu mahakama ikasema maovu ambayo Chebukati alifanya ndiyo halali,” amesema Odinga, akiongezea kwamba “na mimi nikasema kwamba kama sisi hatutoshi, wakenya wote ambao walijitokeza kupiga kura hawana maana na tukasema tutakaa chini tuone vile tutaendelea”.

 

Odinga amekuwa akiishutumu kila taasisi ya serikali na jumuiya ya kimataifa, akidai kwamba “walishiriki kumnyima ushindi”.

 

“Nimekaa kimya sio kwamba nimeridhika. Hapana! Nimekaa kimya kwa sababu nimeona maovu yametendeka. Nahisi vile nyinyi mnahisi.”

Odinga ameilaumu serikali ya Ruto kwa kuendelea kupanda kwa gharama ya maisha.

EXCLUSIVE: SHABIKI SIMBA ALIYETREND kwa KUSHANGILIA GOLI la AL HILAL vs YANGA na KUPEWA SHAVU SUDAN

Leave a Comment