×

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa EU Kukubaliana Kufundisha Askari 15000 wa Ukraine

EU inatarajiwa kutoa mafunzo kwa askari 15000 wa Ukraine

MAKUBALIANO ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi zinazounda Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kukubaliana kutoa mafunzo kwa askari 15000 wa Ukraine ili kusaidia nchi hiyo kuweza kukabiliana na vita inayoendelea nchini mwao dhidi ya Urusi.

 

Mafunzo hayo yanatarajiwa Kwenda sambamba na msaada wa Euro Milioni 500 ambazo zitatumika kwa ajili ya kununulia zana za kivita ili ziweze kusafirishwa kuelekea Kyiv kupitia Luxembourg.

Mafunzo yanatarajiwa kuambatana na msaada wa zana za kivita

Viongozi wawili wa juu wa Umoja wa Ulaya wamesema kuwa mafunzo hayo yanatarajiwa kuanza katikati mwa mwezi Novemba na yanatarajiwa kufanyika katika mipaka ya Mataifa yanayounda Umoja wa Ulaya kwenye nchi za Poland na Ujerumani.

 

Siku za nyuma baadhi ya mataifa yamekuwa yakivifunza vikosi vya Ukraine namna ya kutumia baadhi ya silaha jambo ambalo limebainishwa kuwa litaendelea kama kawaida.

Leave a Comment