
KAMPUNI ya Puma Energy Tanzania, mapema leo imezindua mitungi mipya ya gesi yenye ujazo tofauti huku ikizingatia zaidi hali ya Mtanzania wa chini kabisa.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Puma, Lameck Hiliyayi amesema kuwa mitungi hiyo ya gesi imezingatia kuanzia usafi wa jikoni kwa jinsi yalivyotengenezwa lakini pia kumrahisishia mtumiaji kutolipa gharama za usafiri anapoletewa nyumbani.

Lameck aliongeza kuwa mitungi hiyo itakuwa na njia ya kisasa katika utumiaji kwani mtumiaji ataweza kutumia simu yake ya mkononi kwa kupakua App ya Puma Gas au kwa njia ya USSD, ambayo itakurahisishia wewe mtumiaji kuletewa popote ulipo bila malipo ya usafiri na hata kama kuna tatizo lolote litakalotokea wanaweza kufika nyumbani kwako kwa haraka sana.
” Ukweli ni kwamba kama mnavyoolewa Puma, wako vizuri sana katika bidhaa zao, hivyo mitungi ambayo imezinduliwa leo, ya kisasa na sio ya kulipuka au kuleta matatizo kwenye nyumba kwani imetengenezwa madhubuti kabisa na bei yake ni rafiki kwa mtumiaji,” alisema Lameck.