×

Watu 11 Wakamatwa Kwenye Maandamano Nchini Ufaransa

Raia nchini Ufaransa wameandamana huku 11 kati yao wakikamatwa na Polisi

WATU 11 wamekamatwa na Polisi wa Ufaransa katika maandamano ya maelfu ya watu wakipinga mfumuko wa bei, ongezeko la bei la mafuta na gesi pamoja na nyongeza ya mshahara.

 

Taarifa hiyo imetolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ufaransa na kueleza kuwa maandamano hayo yamefanyika katika Mji Mkuu wa Ufaransa, Paris ambapo waandamanaji walivunja madirisha ya maduka.

 

Wizara hiyo imebainisha kuwa watu 13,000 waliingia katika mitaa ya Mji wa Paris na kuanzisha maandamano hayo huku wengine wakitoka katika viwanda na vyama vya siasa vya mrengo wa kushoto.

Maandamano ya raia nchini Ufaransa

Video zilizosambaa mitandaoni zilionesha, Polisi wakikabiliana na waandamanaji huku watu waliovaa kofia nyeusi wakionekana wakivunja madirisha ya maduka.

 

Hapo awali, maandamano hayo yalikuwa madogo lakini wanasiasa wa upinzani wakachochea maandamano hayo na kufanya yawe makubwa zaidi.

 

Kwa upande wa chama cha wafanyakazi wenye misimamo mikali cha CGT kimetoa watu 70,000 walioshiriki katika maandamano hayo.

 

Usafiri wa treni za kikanda ulisitishwa kwa muda kadhaa wakati vyama vya wafanyakazi vilipoitisha mgomo wa nchi nzima, lengo likiwa ni kutaka kunufaka kiuchumi.

 

Serikali ya Ufansa imekuwa kwenye hatari ya kiuchumi kutokana na kampuni kuu ya mafuta ya TotalEnergies kuelemewa kwa mwezi mmoja katika usambazaji wa petroli nchini humo.

 

Usafiri wa treni za kikanda ulisitishwa kwa muda

Hayo yamejiri wakati ambao serikali ya nchi hiyo ikipanga kupitisha bajeti ya mwaka 2023 kwa kutumia mamlaka maalum ya kikatiba ambayo itaweza kuruhusu kupitisha kura bungeni kwa ajili ya kujadili suala hilo.

 

Imeandaliwa na Sanifa Khalifa kwa msaada wa mtandao

Leave a Comment