×

Wizara ya Ardhi DSM Yaendelea Kutekeleza Maagizo ya Waziri Angelina Mabula, Yafanya Clinic Ya Ardhi

Kamishina wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Dar es salaam Bw. Idrisa Kayera (kushoto) akimkabidhi mwananchi hati yake ya umiliki ardhi.
Wizara ya Ardhi mkoa Dar es salaam imeendelea kutekeleza agizo la waziri Mwenye dhamana ya Wizara hiyo Dr. Angelina Mabula ambaye ameagiza kuendeshwa kwa clinic za elimu ya Ardhi katika maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam na Tanzania Kwa ujumla.
Akizungumuza Katika viwanja vya shule ya msingi Bunju, Kamishina wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Dar es salaam Bw. Idrisa Kayera amesema Zoezi hilo limekua na mafanikio makubwa ambapo linaambana na Utoaji elimu na utatuaji wa changamoto na migogoro yote ya Ardhi na viwanja katika kata na viunga vyote vya Jiji la Dar es salaam.
 Kamishina Kayera amesisitiza kuwa zoezi la upatikanaji wa Hati za viwanja Sasa ni rahisi na haraka hivyo wananchi wasisite kulipia gharama za umilikishwaji Ardhi ili kuzipa thamani Ardhi zao Kwa  maendeleo yao na taifa Kwa ujumla.
Kamishina wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Dar es salaam Bw. Idrisa Kayera (kushoto) akimkabidhi mwananchi hati yake ya umiliki ardhi.
Katika hatua nyingine Kamishina Kayera ametoa wito Kwa wananchi kutumia kipindi hiki Cha msamaha wa  malimbikizo ya Kodi ya majengo uliyotolewa na Serikali kuweza kulipia Kodi zao ili kuiwezesha Serikali kutekeleza miradi mingine ya maendeleo.
Kwa upande wao wananchi waliopokea hati zao katika kata ya Bunju wameishukuru serikali ya Rais Mama SAMIA Suluhu kupitia Wizara ya Ardhi Kwa kurahisisha huduma za umilikishwaji  na utoaji Hati zinazoambatana na clinic ya elimu ya Ardhi Kwa wananchi kiasi Cha kupunguza gharama na urasimu uliokua umezoeleka juu ya upatikanaji wa Hati hizo.
Baadhi ya wataalamu wa TEHAMA kutoka Wizara ya Ardhi wakichakata hati za umiliki ardhi kwa ajili ya kuwapatia wananchi.
Huduma ya Clinic za elimu ya Ardhi na ugawaji wa Hati utaendelea kutolewa katika maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam na wananchi wanaombwa kutoa ushirikiano wa kutosha wanapotangaziwa kupitia ofisi zao za  Kata pamoja na Serikali za mitaa.
Kamishina wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Dar es salaam Bw. Idrisa Kayera (kushoto) akimkabidhi mwananchi hati yake ya umiliki ardhi.

Leave a Comment