×

Jumuiya ya Wazazi CCM Temeke Ilivyopata Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji, Wenye Nongwa Waonywa

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Temeke, Hamis Slim Hamis akizungumza na wajumbe kwenye uchaguzi huo mdogo.

 

 

Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Temeke Dar, baada kuwapata viongozi wake wa ngazi za juu akiwemo Hamis Slim Hamis aliyeibuka Mwenyekiti kwenye uchaguzi uliofanyika mwezi uliopita wikiendi iliyopita uongozi huo ukiongozwa na Mwenyekiti huyo mpya wamefanya uchaguzi mdogo kwa ajili ya kuwapata wajumbe wa kamati ya utekelezaji.

Wajumbe wakipiga kura.

 

Uchaguzi huo ulifanyika Ukumbi wa Taifa uliopo Temeke Wailes Jijini ambapo walipatikana wajumbe hao huku mwenyekiti Hamis Slim akiwaonya wajumbe wenye nongwa baada ya watu wao kushindwa kwenye uchaguzi huo mdogo kuwapa ushirikiano wajumbe waliochaguliwa kwenye uchaguzi huo.

 

Baada ya uchaguzi huo ulifanyika kwa kupigiwa kura za hadharani wajumbe hao walipatikana na wajumbe wote walilidhia na kuahidi kufanyakazi na kuwapa ushirikiano wajumbe hao.

Wajumbe wakifuatilia kinachoendelea.

 

Akizungumza baada ya uchaguzi huo, Hamis Slim alisema uchaguzi ndani ya wilaya na jumuiya hiyo umemalizika na kama kulikuwa na watu wana kambi zao kambi zote zivunjwe sasa washirikine kuwahudumia wananchi kwa kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi kama walivyowaahidi wapiga kura na wananchi kwa ujumla ili tukijenge chama hicho.

Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Temeke, Bi. Lawama Mohammed Mikidadi aliyefika kushuhudia uchaguzi huo akisifia mbele ya wanahabari jinsi ulivyofanyika kwa haki na uwazi.

 

 

Naye Mjumbe wa Halmashauru Kuu Wazazi na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mabatini Kata ya Tandika, Shariff Mustapha Jumbe amesema anawapongeza wajumbe wote kwa ushirikiano mzuri wa wajumbe walioshiriki zoezi la kuichagua kamati hiyo kwa hali ya amani na furaha walioionesha baada ya kuwapata viongozi wa kamati hiyo.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Temeke, Hamis Slim Hamis akizungumza na vyombo vya habari baada ya uchaguzi huo.

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Temeke, Bi. Lawama Mohammed Mikidadi amesema yeye ameshiriki kwenye baraza hilo la wilaya kama mwalikwa na kuhakikisha mambo yanakwenda sawa.

Katibu wa CCM Wilaya ya Temeke Kite Adam ambaye naye alifika kuangalia uchaguzi huo unavyoendeshwa.

 

Lawama ameupongeza uchaguzi huo uliokuwa na watu sita walioteuliwa kuwania nafasi hiyo ambapo waliochaguliwa ni wanne wanawake wawili na wanaume wawili jambo alilosema limezingatia vizuri kabisa usawa wa jinsia.                                                                                                                  HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY /GPL 

Leave a Comment