
IDADI ya watu waliofariki dunia kutokana na Kimbunga cha Sitrang nchini Bangladesh imeongezeka na kufikia 28 huku mamilioni ya watu wakikosa huduma ya umeme.
Idadi hii imeongezeka baada wafanyakazi wa uokoaji wa Bangladesh kuipata miili ya wafanyakazi wanne waliotoweka kwenye boti.
Kimbunga Sitrang kilipiga Oktoba 24, 2022 katika maeneo ya Kusini mwa Bangladesh huku serikali ikieleza kuwa takribani nyumba 10,000 na mazao yaliyopo kwenye mashamba makubwa yakiharibiwa na kusababisha mfumuko wa bei ya vyakula.
Kimbunga ni tishio katika eneo hilo lakini wanasayansi wanasema huenda mabadiliko ya hali ya tabia nchi ikawa sababu ya kutokea mara kwa mara kwa dhoruba hizo.

Kuna kimbunga kingine kilitokea mwaka 2016 ambapo watu watano walifariki dunia nchini Bangladesh na maelfu yao wakiachwa bila ya makazi ya kuishi.
Kimbunga hicho kilikuja na upepo mkali pamoja na mvua kubwa zilizong’oa miti na baadhi ya nyumba kuporomoka huku bandari nyingi zikifungwa.
Imeandaliwa na Sanifa Khalifa kwa msaada wa mtandao