×

Game Super Market Kufunga Maduka Yake Nchini Tanzania

Game SuperMarket

KAMPUNI ya Massmart kutoka Afrika Kusini inayomiliki maduka ya Game imesema Desemba 25, 2022 ni mwisho wa maduka yake kutoa huduma Tanzania.

 

Massmart imefikia hatua hiyo ikiwa ni miezi 12 ya kujaribu kuuza maduka hayo nchini Nigeria, Ghana, Tanzania, Kenya na Uganda kwa wawekezaji wapya wa ndani bila mafanikio.

 

Kampuni hiyo inasema kwa sasa wako kwenye hatua za haraka kuanza uuzaji wa jumla wa bidhaa zilizopo katika maduka yote kwenye nchi husika.

Leave a Comment