
WOLVERHAMPTON Wanderers imemtambulisha rasmi Julen Lopetegui raia wa Hispania na aliyewahi kuwa Kocha mkuu wa klabu ya Reala Madrid pamoja na Sevilla kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo.
Lopetegui ambaye hivi karibuni ametimuliwa kazi kutoka klabu ya Sevilla anaungana na Kocha mwenzie raia wa Hispania Unai Emery ambaye amejiunga na klabu ya Aston Villa kuchukua nafasi ya Steven Gerrard aliyetimuliwa na klabu hiyo kufuatia mfulululizo wa matokeo mabovu.
Lopetegui anachukua mikoba ya Bruno Lage ambaye alitimuliwa klabuni hapo Oktoba 2 baada ya kushinda mchezo mmoja tu kati ya michezo yake 15 ya mwisho.
Klabu ya Wolves imekuwa ikipitia kipindi kigumu cha matokeo uwanjani licha ya timu hiyo kuwa na nyota wengi akiwepo mshambuliaji wa zamani wa Chelsea na Atletico Madrid Diego Costa