
Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Albert Chalamila idadi ya waliofariki yafikia 19, majeruhi 26.
Taarifa hiyo imetolewa mbele ya Waziri mkuu wa Tanzania ambae alifika mkoani humo muda mfupi uliopita.
Naye waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa aliongeza kuwa inawezakana marubani wakawa miongoni mwa waliofariki katika ajali hiyo.
” Kwa namna ndege ilivyofika chini, sina uhakika lakini tutapata taarifa wale ma rubani wetu wanaweza kuwa kati ya wale 19” alisema Waziri mkuu Kassim Majaliwa
Precision Air ndiyo shirika kubwa la ndege la binafsi la Tanzania na kwa sehemu inamilikiwa na Kenya Airways. Ilianzishwa mnamo 1993 na inaendesha safari za ndege za ndani na kikanda.


