×

Droo ya Hatua ya 16 Bora ya Uefa Yatangazwa Rasmi, Vigogo Kuumana

Droo ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya (UEFA)

DROO ya hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya UEFA imetangazwa leo huku ikishuhudiwa baadhi ya miamba ya soka barani humo ikikutana mapema.

 

Katika Droo hiyo Mabingwa wa muda wote wa mashindano hayo klabu ya Real Madrid imepangwa kumenyana na Liverpool ya nchini Uingereza huku Mabingwa wa Ujerumani klabu ya Bayern Munich akimenyana na Paris Saint Germain ya nchini Ufaransa.

PSG itamenyana na Bayern Munich ya nchini Ujerumani

Kwa upande mwingine klabu ya Chelsea yenyewe itaanzia ugenini katika Uwanja wa Signal Iduna Park dhidi ya klabu ya Borussia Dortmund kabla ya kumalizia mchezo wa marudiano katika Uwanja wa Stamford Bridge jijini London, Uingereza.

Real Madrid itacheza dhidi ya Liverpool ya nchini Uingereza

Michezo yote hiyo inatarajiwa kuanza kuchezwa Februari 14 na 15 mwaka 2023.

Leave a Comment