×

Waajiri Waaswa Kuwasilisha Michango ya Wanachama kwa Wakati

Baadhi ya wanachama wakiwa katika mkutano huo.

 

 

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umewataka  waajiri ambao wanachelewesha   michango ya watumishi kunasababisha  tozo ya ucheleweshaji wakati wa kulipa mafao kwa wanachama.

Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Kanda ya Temeke, Rajabu Kinande (kushoto) akizungumza.

 

 

Hapo yamesemwa leo Novemba 7na Meneja wa PSSSF Temeke,Rajabu Kinande Jijini Dar es Salaam, wakati wa Mkutano Mkuu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Dares Salaam DCPC.

Mkutano huo ukiendelea.

 

 

Amesema kitendo cha mwajiri kuchelewesha mchango huo kunaathiri mafao ya wastaafu hivyo kuchukua muda mrefu wakati wa kufanya malipo.

Mkuu wa Mawasliiano TCRA, Semu Mwakanjala akizungumza kwenye mkutano huo.

 

 

“Ili kupunguza malalamiko ni vyema waajiri kutimiza wajibu wao kisheria wa kulipa michango ya watumishi wake ndani ya mwezi mmoja baada ya mwisho wa mwezi husika” amesema Kinande.

 

 

“Utaratibu wa kufanya malipo upo kiteknolojia ambapo kumbukumbu za malipo zitahifadhiwa kwahiyo mwajiri ananuwezo wa kutengeneza namba za kumbukumbu ya malipo itayomuwezesha kulipa michango na kupata risiti kupitia mtandao.

 

 

Pia Kinande amesema wastaafu wengi wanachelewa kupata mafao yao kutokana na kuchelewesha taarifa zao za kustaafu kabla ya miezi sita.

 

 

“Niendelee tu kusema  hakuna watumishi wanaowafanyia mpango wastaafu wengine kupata mafao mapema badala yake uwahishaji wa taarifa zao ndio unawasaidia kupata stahiki zao mapema.

 

 

“Mara  baada ya kupata taarifa hiyo, mtumishi anatakiwa kuanza kufuatilia mafao yake kwa kupeleka taarifa zote muhimu katika ofisi hizo ili zianze kufanyiwa kazi ikiwemo kufuatilia kama waajiri wamechangia miezi yote kama inavyotakiwa na sheria amesema.

 

 

Nae Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini( TCRA) Semu Mwakyanjala, amesema takwimu sasa zinaonesha matumizi ya intaneti yameongezeka kwa asilimia 4.2 kutoka watumiaji 29,858,759 mwaka 2021 hadi kufikia 31,122,163 Septemba 2022.

 

 

“Asilimia 95 ya watanzania wapo kwenye maeneo yenye mtandao weye uwezo wa kutoa huduma za simu za sauti na ujumbe mfupi yaani meseji.”

 

 

“Pia asilimia 68 wapo kwenye maeneo ya mtandao unaowezesha huduma za internet ya kasi ya 3G na asilimia 45 wapo kwenye maeneo yenye mtandao wa 4G,” anasema.

 

 

Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania ( UTPC) Deogratius Nsokolo, amesema watahakikisha DCPC inakuwa kinara wa klabu zote zilizopo nchini, kwani wadau wanaitazama Dar es Salaam zaidi kuliko mikoa mingine.

 

 

“Nimefika hapa kuona mkutano MKuu unavyofanyika, nimekuta watu wana ari, sikutegemea kama ningekuta ari hii, sikuwahi kuona Dar es salaam imesimama, hivyo nina matumaini makubwa kuona Dar es Salaam imebadilika na Dar es Salaam mpya unakuja, hivyo basi naupongeza uongozi mpya kwa kazi kubwa ambayo wanaifanya.

 

 

“Uwepo wa wadau haotadhiri sisi kuwasemea imani kwa wadau iongezeni ili wapatikane wadau wengi zaidi,” alimaliza kusema Nsokolo.

Leave a Comment