
Nyota wa timu ya Young Africans SC, Stephan Aziz Ki na Clatous Chama wa Simba SC wamefungiwa michezo mitatu (3) na kutozwa faini ya Tsh 500,000 (laki tano) kwa kosa la kukwepa kusalimiana na wachezaji wa timu pinzani kabla ya kuanza kwa mchezo kati ya Timu hizo.

Wachezaji hao kwa nyakati na mazingira tofauti walionekana kufanya hila kwa kusubiri nje ya kiwanja ili kusubiri zoezi la kusalimiana likamilike ndipo waingie kiwanjani.
Adhabu hii ni kwa uzingativu wa Kanuni 41:5(5.4) ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti kwa Wachezaji.
