×

Majaliwa Apokewa Jeshini, Kuanza Mafunzo Chuoni Wilaya ya Handeni Mkoa wa Tanga

Kijana Majaliwa Jackson Samweli ambaye alionesha ushujaa mkubwa wa kuokoa abiria katika ajali ya ndege ya Precision Air iliyotokea Bukoba, tayari amepokelewa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

 

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, SACF Puyo Nzalayaimisi, imeeleza kuwa kijana Majaliwa, amepokelewa ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan.

 

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Majaliwa anatarajia kuanza mafunzo ya Zimamoto na Uokoaji pamoja na ya uaskari katika Chuo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kilichopo Chongo Wilaya ya Handeni Mkoa wa Tanga.

 

Pichani ni Jackson Samweli akiwa ofisi ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kagera akipokelewa na Kamanda wa Mkoa kamishna msaidizi mwandamizi Zablon Muhumha.

KIJANA SHUJAA ALIYEWAOKOA ABIRIA 24 APEWA MIL1, AMWAGA MACHOZI MBELE YA WAZIRI MKUU..

Leave a Comment