
Novemba 16, 2022.Kampuni inyoongoza ya Mawasiliano na Teknolojia, Vodacom Tanzania Plc imezindua vipanga njia (Routers) vya 5G Fixed Wireless Access ambavyo vitaunganisha nyumba na biashara kwenye mtandao wa 5G unaounganisha wateja kwa haraka na urahisi zaidi.

Mnamo mwezi Septemba, Vodacom Tanzania ilizindua mtandao wa kwanza wa 5G nchini, kuashiria hatua kubwa ya maendeleo katika uvumbuzi na teknolojia. Kupitia 5G, wateja sio tu watafaidika na kasi ya haraka na yenye utulivu bali pia watanufaika na matumizi ya teknolojia zinazoibuka kama vile matumizi ya Intaneti na akili bandia (Internet of Things). Hivi karibuni ilifanikiwa kununua mawanda (Spectrum) ambapo inakusudia kuyatumia kupanua mtandao na uwekezaji, ikijumuisha usambazaji wa mtandao wenye kasi wa 5G.

Katika mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Vodacom Business, Arjun Dhillon alisema, “pamoja na kwamba 5G imezinduliwa nchini, bado haijaanza kutumiwa na wateja wetu na wafanyabiashara wengi kutokana na ukweli kwamba vifaa vingi vya intaneti vinakosa uwezo wa kuunganishwa kwenye 5G, kwa hivyo leo tunafurahia kuzindua vipanga njia vyetu vya 5G ambavyo vitawezesha wateja wetu kufurahia intaneti yenye kasi ya 5G.”

Kupitia uwepo wa 5G, wafanyabiashara na wateja wa kampuni hiyo watapata nafasi ya kutumia intaneti yenye uwezo mkubwa zaidi, na muda mchache wa kusubiri ambao utasaidia ubunifu zaidi na hivyo kujenga Tanzania iliyo bora na iliyounganishwa na dunia nzima.
“Huduma ya 5G kwa nyumbani na kwenye biashara, inaendeshwa na mtandao pekee nchini unaompa nafasi mtu yeyote anayetaka muunganisho wa haraka kwenye mtandao, ambao pia unaruhusu kutiririsha (stream) bila kukata, kupata michezo (games) au kufanya kazi kwa urahisi. Kutumia 5G kwenye biashara kunamaanisha tija ya hali ya juu, ufanisi na matumizi miunganisho zaidiwakati kwa nyumbani inamaanisha nyumba bora (Smart homes) na matumizi bora ya mtandao,” aliongeza Arjun.
Kulingana na Mkurugenzi huyo, vipanga njia vya 5G kwa ajili ya biashara tayari viko sokoni ikiashiria muungano wa kipekee na utendajikazi wa haraka na kupitia muunganisho usiotumia waya (Wireless WAN) na ubunifu wa hali ya juu katika maeneo ya kudumu na ya muda, magari, na kwingineko.
Pamoja na upanuzi wa huduma za 5G kitaifa, vipanga njia vyetu vya 5G vinatoa suluhisho kwa biashara kuaminika zaidi kuliko hapo awali. Makampuni yanaweza kuona thamani ya muda kutoka kwa mipango yao ya matumizi ya intaneti na akili bandia (IOT), fursa kubwa zaidi ya kuondoa gharama za uunganishwaji na matengenezo kwa kutumia waya, kuongezeka kwa muda wa mtandao na uthabiti unaohusisha na matumizi ya bila waya.
Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Chapa na Mawasiliano wa Vodacom Bi. Warda Kimaro alisema 5G itaongeza kwa kiasi kikubwa kasi na mwitikio wa mitandao isiyotumia waya na kuipanua ili kuwezesha wateja maelfu kuunganishwa.
“Ili kupata uzoefu wa mabadiliko yenye nguvu za 5G nyumbani na kwenye biashara zao, wateja wetu wanaweza kuwasiliana nasi kupitia njia mbalimbali kama vile barua pepe, kupiga simu, maduka au tovuti yetu,” alisema Warda huku akitoa wito kwa wateja na wafanyabiashara kufika Vodacom ili kuagiza vipanga njia vya 5G.
Vifurushi tofauti vya 5G vinavyotoa kasi ya hadi 350Mbps na ada ya kila mwezi ya data vitapatikana kwa wateja ili kukidhi mahitaji yao mahususi. Kwa sasa, mtandao wa 5G unapatikana Dar es salaam pekee huku kukiwa na mipango ya kupanua teknolojia ya 5G hadi takriban maeneo 230 nchini, yakiwemo Arusha, Dodoma, Mwanza, Iringa, Kagera, Zanzibar na Mbeya.
Kuhusu Vodacom Tanzania:
Vodacom Tanzania PLC ndiyo kampuni inayoongoza nchini ya kutoa huduma za simu na za kifedha kwa simu za mkononi. Tunatoa huduma mbalimbali za mawasiliano kwa wateja na makampuni – ikiwa ni pamoja na sauti, data na ujumbe, video, wingu na upangishaji (Cloud and Hosting), suluhu za simu na huduma za kifedha – kwa zaidi ya wateja milioni 15.
Vodacom Tanzania na kampuni tanzu ni sehemu ya Vodacom Group iliyosajiliwa nchini Afrika Kusini, ambayo kwa upande wake inamilikiwa na Vodacom Group Plc ya Uingereza. Imesajiliwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) kwa nambari ya usajili ISIN: TZ1886102715 Jina la Hisa: VODA.
Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea tovuti yetu: : www.vodacom.co.tz