×

UVCCM Sengerema Kuachana na Ombaomba

Kutokana na Jumuiya ya Vijana za Chama Cha Mapindizi UVCCM kutokuwa na vitega uchumi kwa ajili ya kuendesha jumuiya hiyo, Baraza Kuu la Jumuiya hiyo wilayani Sengerema wamekubaliana kwa kauli moja kuanzisha miradi ya maendeleo ili kuondokana na hali ya kuombaomba ili kukidhi mahitaji yake.

Kauli hiyo imetolewa jana Novemba 16, 2022 na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Patrick Mundeba kwenye kikao hicho kinachofanyika wilayani humo.

Amesema moja ya mkakati wake ilikuwa ni kuweka jumuiya kwenye mstari wa maendeleo ikiwa moja ni kuanzisha miradi ya maendeleo ili Jumuiya hiyo iweze kujiendesha.

 

Hivyo anashukuru Baraza hilo kupitisha ajenda hiyo ambayo ilikuwa ni muhimu kupishwa na baraza hilo kilichobaki ni kuweka mkakati wa namuna nzuri ya kuanzisha miradi hiyo.

Jumuiya ya umoja wa vijana wa UVCCM wilaya ya Sengerema ilikuwa haina mradi wowote wa maendeleo hivyo ni mwanzo wa jumuiya hiyo kuwa na ukomavu katilka kujisimamia.

Mmoj wa wajumbe wa baraza hilo Matias Gerevaz amesema kuanzisha miradi ya maendeleo ya Jumuiya imeonyesha ukomavu hivyo tunatakiwa kwa pamoja kulikamilisha jambo hili.

Leave a Comment