
Dar es Salaam: 8 Desemba 2022, Washindi wa Promosheni ya WAKISHUA TWENZETU QATAR na Hisense, wamerejea nchini Tanzania wakitokea Qatar kushuhudia baadhi ya mechi za kombe la dunia.
Ikumbukwe safari hii imelipiwa na Tigo Tanzania kwa kushirikiana na Hisense, kupitia Promosheni yake ya WAKISHUA TWENZETU QATAR na Hisense ambapo walipatikana jumla ya washindi 50 waliokwenda Qatar huku baadhi wakijishindia bidhaa za ndani kutoka Hisense ambazo ni friji, spika za muziki wa kisasa (SubWoofer), smart Tv, pamoja na microwave.

Akizungumza baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) Meneja wa Wateja Maalum Tigo Pesa, Mary Rutta amesema;
“Hili ni kundi la mwisho la washindi wote 50 tuliowapeleka Qatar kushuhudia mechi mbalimbali za kombe la dunia kama mnavyotuona tumerudi salama na wateja wetu hawa wamepata ‘experience’ ya kutosha huko maana wengi hii ni mara yao ya kwanza.

Promosheni hii inaendelea ambapo sasa inakuja kivingine na Shinda Ndinga la Kishua hivyo endeleeni kufanya miamala mingi iwezekanavyo kama vile kulipa bili, mikopo ya bustisha, malipo ya kiserikali, kutuma na kupokea pesa kutoka benki n.k kupitia Tigo Pesa au piga *150*01#.
Ili kuibuka mshindi wa zawadi za pesa taslimu (milioni 1 kila wiki, milioni 5 kwa mwezi wa Disemba na zawadi kuu za pesa taslimu milioni 10 na milioni 20), vifaa vya ndani vya Hisense na gari jipya kabisa aina ya Toyota Rush”. Alimaliza kusema Mary.

Naye mmoja wa washindi hao waliorejea ambaye amejitambulisha kwa jina la Baraka mkazi wa Arusha, ameipongeza kampuni ya Tigo kwa zawadi hiyo kubwa waliyotoa kwa wateja wao.
“Nawasihi wateja wa Tigo Pesa waendelee kufanya miamala kwa wingi maana ndio siri pekee ya Ushindi na mimi nitaendelea kufanya miamala maana baada ya kutoka Qatar naweza nikashinda tena zawadi nyingine zinazoendelea kutolewa au hata zawadi kubwa kabisa ya gari aina ya Toyota Rush”.