×

Happy New Year Wananchi… Waibuka na Ushindi Dhidi ya Mtibwa Sugar, Aziz Ki Atupia

Stephane Aziz Ki akifanya yake dhidi ya dhidi ya Mtibwa Sugar.

WANANCHIIIII… Happy New Year 2023. Mashabiki wa Yanga SC, wamepewa zawadi ya mwaka mpya na timu yao baada ya jana kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Manungu, Morogoro.

Dakika 45 za mwanzo, zilikamilika kwa ubao wa Uwanja wa Manungu kusoma Mtibwa Sugar 0-1 Yanga, huku kazi ikiwa kubwa upande wa ulinzi wa Mtibwa Sugar.

Shukrani kwa Stephane Aziz Ki ambaye alifunga bao hilo dakika ya 26 kwa mkwaju wa faulo ambao ulimshinda kipa wa Mtibwa Sugar, Razack Kimweri, ukamgonga na kujaa wavuni.

Aziz Ki alipewa jukumu la kupiga faulo na alifanya hivyo dakika ya 24, 35 na 45. Pigo lake la dakika ya 45, Kimweri alifanikiwa kuokoa na kulifanya lango lake kuwa salama.

Kwa Mtibwa Sugar, ni David Kameta huyu alifanya jaribio dakika ya 41 halikulenga lango sawa na lile la Ismail Aidan dakika ya 42.

Kipa wa Yanga, Djigui Diarra, shuti moja la moto alikutana nalo dakika ya 39 ambapo alifanikiwa kuokoa na kuweka lango lake salama. Hadi dakika 45 za kwanza zinamalizika, matokeo yalikuwa Mtibwa 0-1 Yanga.

Kipindi cha pili ambapo Mtibwa ilikuwa inasaka bao la kusawazisha, juhudi zao hazikuzaa matunda kwani ubao haukubadilika na kuifanya Yanga kusepa na pointi zote tatu.

Yanga ushindi huo umewafanya kufikisha pointi 50 baada ya kucheza mechi 19 za Ligi Kuu Bara msimu huu, bado wapo kileleni wakiiacha Simba pointi sita. Simba inazo 44.

DIAMOND AKATIWA UMEME KATIKATI YA SHOW RAMADA RESORT| Cheers 2023


 

Leave a Comment