×

Musonda Akutana Na Kigingi Cha Kwanza Yanga, Kocha Atoa Onyo kwa Wachezaji

Kennedy Musonda.

KATIKA kuhakikisha anatengeneza nidhamu ya mastaa wake, Kocha Mkuu Yanga Mtunisia Nasreddine Nabi ametembeza mkwara mzito kwenye kambi ya timu hiyo.

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu wawatambulishe wachezaji wao wawili ambao wamewasajili katika dirisha dogo ambao ni Kennedy Musonda, Mudathir Yahya na Metacha Mnata.

Yanga imewasajili wachezaji hao kwa lengo la kutetea makombe yao ya msimu huu Ligi Kuu Bara, Kombe la FA na kufika mbali katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Akizungumza na Championi Jumatano, Nabi alisema kuwa wachezaji wake wafahamu kuwa katika timu hiyo, hakuna mchezaji aliyekuwa juu ya klabu ni vyema kila mmoja kufuata taratibu na sheria zilizowekwa na benchi la ufundi.

Nabi alisema kuwa anataka kutengeneza usawa kwa kila mchezaji, hivyo hilo litawahusisha wachezaji wa zamani na wapya ambao wamesajiliwa na timu hiyo, katika dirisha hilo dogo.

Aliongeza kuwa mchezaji atakayekwenda kinyume cha matakwa yake, basi hatamuangalia usoni, basi atampiga benchi hata kama anapendwa kiasi gani na mashabiki.

“Mashabiki wanapaswa kujua kuwa hakuna mchezaji mkubwa kuliko timu, na kila mchezaji anapaswa kufuata taratibu zote za timu na benchi la ufundi, hilo nilishawaambia wachezaji wangu wote.

“Hivyo basi akitokea mchezaji akaenda kinyume na matakwa yangu sitamuangalia usoni na badala yake nitampiga benchi hata kama anapendwa kiasi gani na mashabiki.

“Ninataka kuona kila mchezaji anafuata taratibu zote za benchi la ufundi, na ili tufanye tufanye vema na kutengeneza umoja wa timu, basi ni lazima wachezaji wote wawe na nidhamu,” alisema Nabi.

STORI NA WILBERT MOLANDI

ISHU YA MORRISON MAAMUZI MAZITO YANGA, MASHINE MPYA SIMBA HADHARANI LEO | KROSI DONGO….

Leave a Comment