Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na ASSAD Associates wameboresha mfumo wa walipakodi kujihudumia wao wenyewe kupitia mfumo wa kidigitali wakiwa katika maeneo yao ya Biashara bila kufika ofisi za Mamalaka ya mapato.
TRA imesema wameona umuhimu wa kushirikiana na ASSAD associates ili kuwapa elimu kama wadau ili kuweza kuwafikia walengwa wote nchini na kusema ni rahisi mfumo huo na salalama kulinganisha na mifumo ya nyuma na unaweza kutoa risiti kidigitali au kujaza taarifa zako na kujipatia TIN namba kidigitali.
Aidha washiriki wa mkutano huo wamesema itawasadia sana na kuepuka vishoka katika kujaza au kutafuta huduma kutoka Mamlaka ya Mapatao TRA. ⚫️ SIKILIZA + 255 GLOBAL RADIO LIVE: http://ndstream.net/globalradio/ ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx