×

Bosi Yanga Atamba Kutaitetemesha Afrika Dhidi ya US Monastir leo

HUKU wakiwa wanashuka uwanjani leo Jumapili usiku kuvaana na US Monastir katika mchezo wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe ameweka wazi kuwa wamepokea maagizo ya Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ya kuwatetemesha Watunisia na kuweka wazi wamejipanga kuitetemesha Afrika.

Yanga ambao wamepangwa Kundi D, leo Jumapili watavaana na US Maonastir katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambao unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Olimpique Rades jijini Tunis, Tunisia.

Kuelekea mchezo wa leo, juzi Ijumaa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa alizitakia kheri Simba na Yanga katika uwakilishi wao kwenye mashindano ya kimataifa wakati wa hotuba yake bungeni, Dodoma.

Akizungumza na Spoti Xtra, Kamwe alisema: “Maandalizi yetu ya mchezo dhidi ya US Monastir yanaendelea vizuri ambapo mpaka sasa tumekamilisha sehemu kubwa ya programu za mazoezi na naweza kusema kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo dhidi ya Monastir ambao ni wazi tunatarajia mchezo mgumu.

“Tumefurahi kupata salamu za kheri kutoka kwa Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu ambaye ametutaka tuitetemeshe Tunisia, sisi tumepokea hayo kama maagizo na tutapambana kuitetemesha Tunisia na soka la Afrika.”

STORI NA JOEL THOMAS, SPOTI XTRA

KIJANA AUAWA KWA KUSUKUMWA GHOROFANI DAR, SUNGUSUNGU WATAJWA KUHUSIKA- ”KICHWA CHOTE KIMEHARIBIKA”

Leave a Comment