
Dar es Salaam 12 Februari 2023: Kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya inayoongoza hapa nchini, Vodacom kwa kushirikiana na Duka la Mr Price na Migahawa ya KFC imezindua ofa ya Valentine ambapo mteja akipata huduma kwa kutumia huduma ya Lipa kwa Simu atapata punguzo la asilimia 10.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa ofa hiyo, Mkuu wa Idara ya Lipa kwa M Pesa alisema Vodacom imekusudia kurahisisha malipo kwaajili ya manunuzi ya bidhaa na huduma mbalimbali haswa katika msimu huu wa Valentine.

Ameendelea kusema kuwa huduma hii inawasaidia wafanyabiashara kuweka vizuri rekodi zao za mauzo na kuwafanya wateja wake wasitembee na pesa taslimu kwa usalama wao haswa kipindi hiki cha Valentine na kuwataka watumiaji wa simu za mkononi kutumia mtandao wa Vodacom ili kupata huduma za Lipa kwa Simu.
Kwa upande wake Meneja wa duka la Mr Price Mliman City Dar, Anna Asajile ametumia nafasi hiyo kuwathibitishia ofa hiyo wateja wote watakaokwenda kwenye maduka yao kufanya manunuzi kwa kutumia huduma ya Lipa kwa Simu.
Naye Meneja wa Mgahawa wa Mr Price, Verynice Temba alianza kwa kuwashukuru Vodacom kwa kuwapelekea ofa hiyo na kuwakaribisha wateja kwenye mgahawa wao na kuwaambia kuwa sambamba na ofa hiyo ya asilimia 10 kutoka Vodacom wana ofa nyingine nyingi kwa wateja wakakaokwenda kupata msosi.
Ukija KFC utapata msosi mzuri na tuna promosheni kibao lakini zaidi tuna promosheni ya Valentine Day ambayo inaitwa ‘Pamoja Meel’. Alisema Meneja Verynice.