×

RC Mgumba Akabidhi Vyandarua Kwa Shule Zote za Mkoa wa Tanga, Ni Vilivyotolewa na Rais Samia

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Omary Mgumba akizungumza katika hafla hiyo kabla ya kuanza kwa zoezi la ugawaji wa vyandarua kwa shule za mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Omary Mgumba akikata utepe kuashiria kuanza kwa zoezi la ugawaji wa vyandarua kwa shule za mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Omary Mgumba (kulia) akikabidhi robota la vyandarua.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Omary Mgumba akiwakabidhi baadhi ya wanafunzi vyandarua Shule ya msingi Mwenge na Mwakinzani Mabawa Tanga Jiji 
Baadhi ya wanafunzi waliohudhuria zoezi la kupokea vyandarua kutoka shule za Mkoa wa Tanga za Mwenge na Mwakinzani Mabawa Tanga Jiji .
Baadhi ya wanafunzi wakiwa wameshikiria vyandarua vilivyotolewa na Uongozi wa Mkoa wa Tanga Chini ya Mkuu wake wa Mkoa Mhe, Omary Mgumba
Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan imegawa vyandarua kwa Shule zote za msingi Mkoani Tanga ikiwa ni mpango wake wa kutokomeza Malaria nchini ifikapo mwaka 2030.
Akizindua mpango huo katika Shule za Msingi Mwenge na Mwakinzani Jijini humo, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba amesema wanafunzi wote wa Shule 1083 zilizopo ndani ya Wilaya nane na Halmashauri 11 watapata vyandarua hivyo.
Serikali Ya Cahama cha Mapinduzi Chini ya Uongozi wa mhe Rais Dkt Samia  imegawa Vyandurua kwa wototo  wote wa Shule za Msingi   zaidi ya shule 1083 Mkoani Tanga Katika Mipango na mikakati yake ya kutokomeza Malaria nchini ifikapo Mwaka 2030 kuwa na kiwango Cha Sifuri
Ugawaji huo unatarajia kuendela katika wilaya zote 8 na Halmasharuo zote 11 za Mkoani Tanga.

Leave a Comment