ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Balozi Mteule, Meja Jenerali Jacob Kingu, naye amefika katika ofisi za Taasisi za Kupambana na Kuzuia Rushwa ( TAKUKURU) jijini Dodoma ili kuhojiwa kufuatia agizo la Rais John Magufuli kuhusu mkataba tata wa Tsh trilioni 1.04 wa ununuzi wa vifaa vya zimamoto.
Mwingine aliyewasili leo Ijumaa, Januari 31, 2020, kuhojiwa na Takukuru ni aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Kangi Lugola, ambaye amefika ofisini hapo mapema leo saa moja asubuhi.
