×

Nabi Aivaa TP Mazembe Kivingine Leo Jumapili Uwanja wa Mkapa, Dar

 Kocha Mkuu wa Yanga NASREDDINE Nabi.

NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga, amesema kuwa watabadili mbinu kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe, huku akija kwa utofauti kulingana na mchezo husika.

Nabi alikuwa benchi kwenye mchezo uliopita ugenini wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika aliposhuhudia ubao ukisoma US Monastir 2-0 Yanga.

Leo Jumapili, Yanga inatarajiwa kucheza mchezo wa pili dhidi ya TP Mazembe ambao wametoka kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Real Bamako.

Akizungumza na Spoti Xtra, Nabi alisema kuwa kila mchezo una mbinu zake tofauti kulingana na aina ya wapinzani wanaokwenda kukutana nao jambo linalowapa nguvu ya kuingia uwanjani kusaka ushindi.

“Ikiwa umepoteza mchezo wa kwanza haina maana kwamba inakuwa ni mwisho wa kuendelea kupambana, yale ambayo yamepita tunasahau na kuanza kufanya maandalizi kwa ajili ya mchezo wetu unaofuata.

“Huwa sipendi kuzungumza sana, ninapenda kuona wachezaji wakicheza na kupata ushindi, kwa namna ambavyo wapinzani wetu watakuwa, ndivyo ambavyo nasi tunapanga kikosi chetu.

“Mbinu ambazo zilitumika ugenini ama kwenye mchezo ambao tulipoteza hatuwezi kuzirudia kwa wakati mwingine, mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,” alisema Nabi.

STORI NA LUNYAMADZO MLYUKA

Leave a Comment