×

Mama Mariam Mwinyi Apongezwa Na UVCCM, Kujipanga Na Matembezi Ya Miaka 60 ya Mapinduzi ZNZ Mwakani

Mke wa Rais Zanzibar, Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mama Mariam Mwinyi 
Mke wa Rais Zanzibar, Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mama Mariam Mwinyi akizungumza na ujumbe uliofika Ofisi za ZMBF, Ikulu Migombani ukiongozwa na  Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa  Ndugu Rehema Omary Sombi 

Mlezi wa Matembezi ya  UVCCM ya  Mapinduzi  ya Zanzibar,  Mke wa Rais Zanzibar, Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mama Mariam Mwinyi  amekutana na Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa  Ndugu Rehema Omary Sombi na ujumbe wake waliofika Ofisi za ZMBF, Ikulu Migombani.
Naye , Makamu Mwenyekiti wa UVCCM  Sombi amempongeza Mama Mariam Mwinyi  kwa kutimiza Mwaka mmoja wa Taasisi yake ya ZMBF,  pia kwa mafanikio ya kazi nzuri kwa kuwawezesha Wanawake wakulima wa mwani,kupambana na  vitendo vya udhalilishaji kwa watoto na kuwa  kinara wa  hamasa katika kushiriki kuhamasisha ufanyaji wa Mazoezi katika  matembezi ya Kila mwisho wa Mwezi kwa mapambano ya Magonjwa yasiyoambukiza.
Aidha, Mama Mwinyi amewataka UVCCM  kuwa Mabalozi wa kitaifa  kwa kuwasemea ,  kukemea Vitendo vya udhalilishaji kwa Watoto  kuibeba kama ajenda ya Kitaifa  wanapozunguka Mikoa ya Unguja, Pemba na Tanzania Bara.
Pia amewapongeza  UVCCM kwa Kusukuma gurudumu la maendeleo  la Jumuiya yao    na Taifa kwa ujumla.
Mke wa Rais Zanzibar, Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mama Mariam Mwinyi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe uliofika Ofisi za ZMBF, Ikulu Migombani ukiongozwa na  Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa  Ndugu Rehema Omary Sombi 
Mama Mwinyi amewataka  kuwa ubunifu  zaidi Katika shamrashamra za matembezi ya kuadhimisha Miaka 60 ya Mapinduzi  ya Zanzibar Mwakani  kwa kuja na mbinu tofauti   kwa kuibua miradi ya vijana kwa maendeleo na kuendelea kuyaenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar .
Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa  Ndugu Rehema Omary Sombi akitoa neno la shukrani.

Leave a Comment