×

AU yaendelea kuzitenga nchi nne za Afrika zinazotawaliwa na jeshi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu akiwa kwenye picha ya pamoja na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa 36 Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika katika Ukumbi wa Nelson Mandela uliopo Makao Makuu ya Umoja huo Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 18 Februari, 2023.

Umoja wa Afrika Jumapili umesisitiza kuwa una sera ya kutovumilia mabadiliko yanayokiuka katiba, huku ukiendelea kusimamisha uanachama wa nchi nne zinazotawaliwa na jeshi

Nchi za Sahel za Burkina Faso, Guinea na Mali vile vile Sudan ziliwekewa vikwazo na taasisi hiyo ya Afrika baada ya mapinduzi ya kijeshi katika miaka ya karibuni, lakini Umoja wa Afrika Jumapili umesema uko tayari kuzisaidia kurejea kwenye utawala wa kidemokrasia

“Mkutano umesisitiza kutovumilia kabisa mabadiliko yanayovunja katiba,” amesema Kamishna wa AU wa masuala ya kisiasa, amani na usalama, Bankole Adeoye.

“Tume iko tayari kuunga mkono nchi hizi wanachama kurejea katika utaratibu wa kikatiba, lengo ni kwamba demokrasia lazima iote mizizi na lazima iimarishwe na kulindwa,” aliuambia mkutano wa waandishi wa habari katika siku ya mwisho ya mkutano wa AU mjini Addis Ababa.

MASHABIKI YANGA WAWAVUA NGUO SIMBA – ”KWA MKAPA HATOKI MTU INATUHUSU SISI”…

Leave a Comment