×

Mwanajeshi Wa JWTZ Aliyemsukuma Trafiki Kwa Gari Afikishwa Mahakamani Kwa Shitaka Hili…

Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ ) namba MT 89487 CPL Hamis Ramadhan (36) jana amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam akikabiliwa na shitaka ya kukataa amri halali.

Mshitakiwa huyo alisomewa shitaka hilo na Wakili wa Serikali, Vailet Kyendesya mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Rahim Mushi.

Kyendesya alidai mnamo Februari 7, mwaka huu, mshitakiwa akiwa eneo la Mlimani City Barabara ya Survey, Kinondoni, Dar es Salaam akiendesha gari namba T. 433 ALB Nissan Patrol alisimamishwa eneo la kivuko cha watembea kwa miguu na Askari Polisi ambapo alikaidi na kuanza kumsukuma Askari kwa gari lake.

Kyendesya alidai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na aliiomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Baada ya kusomewa shitaka hilo, mshitakiwa alikana makosa yake na kuachiwa kwa dhamana.

Kesi hiyo ilihairishwa hadi Machi 6, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Leave a Comment