
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam Bi. Khadija Ally amewataka vijana wa CCM kuendelea kufanya kazi kwa bidii za kukijenga chama hicho hasa wakati huu kuelekea uchaguzi ujao ili kukipatia chama ushindi kwenye chaguzi zijazo za serikali za mitaa.
Akizungumza kwenye mkutano maalum wa uzinduzi wa tawi uliofanyika Wilaya ya Kigamboni Bi. Khadija amewasihi wanachama wa CCM walio na ndoto za kuwa viongozi wa serikali za mitaa kwa mwaka 2024 wajitoke wachukue nafasi hizo kwani wanawajibu wa kuwatumikia wananchi na chama chao.

Katika mkutano huo aidha Bi amempongeza Mwenyekiti wa Tawi la Kigamboni, Ndugu Haji Juma kwa uongozi bora bora wa kuletea maendeleo tawi lake kwa kuanzisha miradi ya kimaendeo inayoliingizia kipato tawi hilo.
“Nimefarijika sana tawi lenu lina miradi ambayo inawaingizia kipato, matawi mengi ni ombaomba hazina miradi, tunataka kutoka huko kwenye siasa za hiyena hiyena na kwenda kwenye siasa za uchumi”

“Haji unafanya kazi nzuri, nipo kwenye mpango wa kushusha mradi mkubwa hapa wa shule za awali za Jumuiya ya Wazazi hapa kwenye tawi lako, mradi ambao utaongeza kipato, utakoa elimu na pia utaleta malezi, na malezi ndiyo sera yetu” amesema Bi. Khadija
Katika hatua hiyo Bi. Khadija ametoa wito kwa baadhi ya viongozi wenye dhamana katika kwenye chama na serikali kuacha fikra za kufikiria uongozi ni ubosi au kuogopwa na kuwataka wauone uongozi ni wito wa kuwatumikia wananchi ili kuwaletea Maendeleo.