×

Mstahiki Meya Ubungo Azitaka Taasisi Kuiga Mfano wa DCB Uboreshaji wa Elimu

Meya wa Manispaa ya Ubungo, Jaffary Nyaigesha ( wa tatu kushoto ) akikata utepe kuashiria makabidhiano ya  msaada Madawati 30 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Isidori Msaki ( katikati ) kwa ajili ya shule ya msingi Kiluvya ikiwa ni muendelezo  wa kampeni ya benki hiyo inayoendelea ya elimu iitwayo ‘Elimu Mpango Mzima na Mama Samia’  shuleni hapo, Kiluvya, Ubungo jijini Dar es Salaam Jana no
Mstahiki Meya wa Ubungo azitaka ya taasisi mbalimbali kuiga mfano wa  Benki ya DCB uboreshaji wa elimu nchini.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo,  Jaffary  Nyaigesha amezitaka  taasisi mbalimbali kuiga mfano wa Benki ya DCB katika juhudi zake za  uboreshaji wa elimu nchini.
Mstahiki meya aliyasema hayo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, wakati akipokea msaada wa madawati 30 kwa ajili ya Shule ya Msingi Kiluvya, iliyo katika Manispaa hiyo jijini Dar es Salaam yaliyotolewa na DCB kupitia kampeni yake ya ‘Elimu Mpango Mzima na Mama Samia’.
Meya wa Manispaa ya Ubungo, Jaffary  Nyaigesha akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya  msaada wa madawati 30 kwa ajili ya shule ya msingi Kiluvya ikiwa ni mwendelezo wa kampeni yake inayoendelea ya elimu iitwayo ‘ Elimu Mpango Mzima na Mama Samia ’ shuleni hapo, Kiluvya, Ubungo jijini Dar es Salaam Jana.
“Kwa kufanya hivi, Benki ya DCB inaunga mkono juhudi za Rais wetu Mpendwa, Mheshiwa Dk. Samia Suluhu Hassan za kuwaletea watu wake maendeleo katika uboreshaji wa elimu nchini”, alisema mstahiki meya.
Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Bwana Isidori Msaki akizungumza mahali hapo alisema,madawati hayo ni sehemu ya madawati 150 yeye thamani ya shs 37,500,000 wanayoyatoa katika Manispaa tano za jiji la Dar es Salaam ikizingatiwa kuwa wao ndio wanahisa  waanzilishi wakati benki ikianzishwa miaka 20 iliyopita.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, Beatrice Dominick akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya msaada wa madawati 30 na Benki ya Biashara ya DCB kwa ajili ya shule ya msingi Kiluvya ikiwa ni mwendelezo wa kampeni yake inayoendelea ya elimu iitwayo ‘ Elimu Mpango Mzima na Mama Samia ’ shuleni hapo, Kiluvya, Ubungo jijini Dar es Salaam jana.x
“Tunajivunia ushirikiano wenye tija na Manispaa hizi kwani kwa kipindi cha miaka 20 kwa mtaji wa shs bilioni 1.7 tuliokuwa nao mwaka 2002, benki imeendelea kukua mwaka hadi mwaka na imeweza kutoa gawio la jumla ya shs bilioni  11.5 kati ya hizo Manispaa zikipokea gawio la shs bilioni 4.55”, alisema Bwana Msaki.
Mkuu wa Shule ya Msingi Kiluvya, Leah Sanga akizungumzia maendeleo ya shule yake wakati wa hafla ya makabidhiano ya msaada wa madawati 30 na Benki ya Biashara ya DCB kwa ajili ya shule ya msingi Kiluvya 
Mkurugenzi huyo alisema, mafanikio haya yanawezekana chini ya uongozi mahiri wa Bodi ya benki hiyo inaoongozwa na mwanamama shupavu Bi. Zawadia Nanyaro.
“Ni matumaini ya DCB kuwa msaada  utazidi kuimarisha mahusiano kwa manufaa ya pande zote mbili, DCB kama mtoa huduma za kibenki na mdau wa maendeleo na kwa manispaa  yako kama wadau wetu muhimu”, alisema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Isidori Msaki akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya msaada wa madawati 30 kwa ajili ya shule ya msingi Kiluvya ikiwa ni mwendelezo wa kampeni yake inayoendelea ya elimu iitwayo ‘ Elimu Mpango Mzima na Mama Samia ’ shuleni hapo, Kiluvya, Ubungo jijini Dar es Salaam Jana

Leave a Comment