×

Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango Kumpokea Makamu wa Rais wa Marekani

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariiki, Dk. Stergomena Taxi akiongea katika mkutano wake na wahariri na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za wizara hiyo jijini Dar.

MAKAMU wa Rais wa Marekani, Kamala Harris, anatarajiwa kuwasili nchini Tanzania kesho Machi 29,  2023 na kupokewa na Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Kamala ambaye atafuatana na mumewe atapokewa rasmi na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan, tarehe 30 Machi 2023 katika Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo wawili hao watafanya mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano baina ya nchi mbili na kushuhudia utiliaji saini wa makubaliano mbalimbali.

Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariiki, Dk. Stergomena Taxi, siku hiyo hiyo, Kmala ataweka shada la maua katika Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam ikiwa ni ishara ya kuwakumbuka waathirika wa mabomu yaliyolipuliwa kwenye Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam mwaka 1998.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari kuhusiana na ugeni huo, Dk. Taxi amesema pia Kamala atatembelea Taasisi ya Tanzania Startup Association ya jijini Dar es Salaam kwaajili ya kukutana na wajasiriamali vijana.

Aidha kiongozi huyo wa juu nchini Marekani atashiriki futari iliyoandaliwa kwa heshim ayake na mwenyeji wake Dk. Samia Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mbali na Tanzania Kamala atazitembelea Ghana na Zambia ikiwa ni ziara ya kiongozi huyo barani Afrika.

#EXCLUSIVE: EBITOKE AFUNGUKA KUIBIWA WAPENZI na MASHABIKI – ”HUYU WAKIMUIBA, WAIBE na MTOTO WANGU”

Leave a Comment