×

Mshambuliaji Aua Watu 6 katika Shule ya Jimbo la Marekani la Tennessee

Mshambuliaji mwanamke Machi 27, 2023 ameua watoto watatu na watu wazima watatu katika shule ya sekondari ya kikatoliki katika jimbo la kusini mwa Marekani la Tennessee, kulingana na maafisa.

Polisi walimpiga risasi na kumuua mshukiwa, ambaye awali walisema alionekana kuwa kijana. Baadaye maafisa walibaini kuwa mshukiwa alikuwa na umri wa miaka 28 na alikuwa mwanafunzi wa zamani katika shule hiyo.

Msemaji wa idara ya polisi ya Nashville, Don Aaron, alisema mshambuliaji alikuwa na bunduki mbili zinazofyatua risasi nyingi kwa muda mfupi na bunduki moja ya mkononi.

Maafisa hawakumtambulisha mshambuliaji na kusema bado hawajabaini nini ilikuwa nia yake.

Polisi waliwataja waliouawa kuwa wanafunzi watatu na wafanyakazi watatu watu wazima.

MO DEWJI APASUA JIPU; KUNA WATU NDANI YA SIMBA WANAKWAMISHA, ANGEKUWA MWINGINE ANGESHAJITOA!

Leave a Comment