×

Rais Samia Amuandalia Futari Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris Ikulu Dar – Picha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mgeni wake Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris wakati akiwasili kwa ajili ya Futari Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Machi, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amuandalia Mgeni wake Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris kwa ajili ya Futari Ikulu Jijini Dar es Salaam Machi 30, 2023.

Rais Samia  akizungumza na Mgeni wake Makamu wa Rais wa Marekani,Kamala Harris wakati wa Futari Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Machi, 2023. Wa kwanza kulia ni Mume wa Makamu huyo wa Rais Douglas Emhoff, Wa kwanza kushoto ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango
Rais Samia  akizungumza na viongozi mbalimbali wakati wa Futari aliyomuandalia mgeni wake Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris.
Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris akizungumza na viongozi mbalimbali katika Futari aliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Machi, 2023.
Rais Samia akimsindikiza mgeni wake Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris mara baada ya Futari.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiagana na mgeni wake Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris pamoja na Mume wa Makamu huyo wa Rais Douglas Emhoff mara baada ya Futari Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Machi, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiagana na Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete mara baada ya Futari Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Machi, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiagana na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa mara baada ya Futari Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Machi, 2023.

PICHA NA IKULU

UGENI MKUBWA: RAIS SAMIA na KAMALA HARRIS WAZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI – DSM…

Leave a Comment